Rais
wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ametakiwa afuate nyayo na dhana ya
utumbuaji majipu ya Rais John Magufuli kwa kuwa imegusa maisha ya
wananchi wanyonge.
Wito
huo ulitolewa juzi na Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana, Jimbo la
Tabora Francis Ntiruka katika mahubiri ya Ijumaa Kuu katika Kanisa Kuu
la Roho Mtakatifu mjini Dodoma.
Askofu
huyo alisema Yesu Kikristo aliteseka hadi kuuawa kwa ajili ya kutetea
haki za wanyonge na vivyo hivyo lazima viongozi wawatetee wanyonge.
Alisema
kifo chake kiliambatana na vipigo vya mateso ya dhihaka nyingi kutoka
kwa watawala waliotaka kujinufaisha wao binafsi pasipo kujali wengine.
“Ni bora ufe kwa ujali wengine kuliko kujinufaisha, alisema askofu huyo ambaye pia ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha St John.
Alimtaka
Dk Shein aliyeapishwa juzi kuwa Rais wa Zanzibar ajipange kuhakikisha
analeta umoja na amani ya Wazanzibari na kutumbua majipu kama
anavyofanya Rais Magufuli.
Alisema
Watanzania wana mateso mengi kama ya umaskini, magonjwa, kuporwa haki
na rasilimali zao jambo alilosema bila kutafutiwa ufumbuzi, malalamiko
yao hayataisha.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )