Chama
cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Mwanza kimeunda kamati kuchunguza
tuhuma dhidi ya baadhi ya walimu wa Shule ya Sekondari Mihama wilayani
Ilemala kujamiiana na wanafunzi wao.
Mwenyekiti
wa CWT mkoani hapa, Sibora Kisheri alisema wameunda kamati hiyo baada
walimu wanane, akiwamo mkuu, Joseph Marifedha kusimamishwa kazi kwa amri
ya aliyekuwa Mkuu wa mkoa huo, Magessa Mulongo kwa tuhuma hizo.
“Haiingii
akili kuona walimu wote wakawa na sifa ya makosa yanayofanana, hivi
hakuwapo hata mmoja aliyeshtukia mchezo huo na kuwashauri wezake,” alisema Kisheri.
Alisema
uchunguzi huo unalenga kubaini kiini cha tuhuma hizo na kuishauri
Serikali na vyombo husika hatua stahiki za kuchukua kuhakikisha kila
upande unatendewa haki.
Aliwaasa walimu kufuata sheria, kanuni na misingi ya kazi kwa kutimiza wajibu na kuepuka mambo yanayokinzana na taaluma hiyo.
Hivi karibuni Mulongo aliwasimamisha walimu hao baada ya kupata taarifa kuwa walikuwa wakijihusisha na vitendo hivyo.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )