WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, amesema Serikali ya Awamu ya Nne iliyokuwa chini ya Rais Jakaya Kikwete haikukomba fedha katika Hazina kama ambavyo baadhi ya wabunge wamedai, hata Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF), lilifanya tathmini na kutoa taarifa safi.
Dk
Mpango alieleza hayo bungeni jana mjini Dodoma, wakati akijibu hoja
mbalimbali zilizotolewa na wabunge wakati wakichangia mjadala wa wizara
mbili zilizo chini ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI) pamoja na Utawala Bora, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma.
Katika
mjadala huo, baadhi ya wabunge walisema Serikali ya Awamu ya Nne,
ilikomba fedha zote Hazina na kusababisha Serikali ya Awamu ya Tano
chini ya uongozi wa Rais John Magufuli, kukuta Hazina haina fedha.
Akijibu
hoja hiyo, alisema hakuna ushahidi ulioitia hatiani Serikali ya Awamu
wa Nne kuhusu kukomba fedha Hazina na kwamba IMF na wadau wengine wa
kimataifa, walifanya tathmini huru ya bajeti na mwenendo wa uchumi
nchini na taarifa yao ya mwisho waliitoa Desemba mwaka 2015.
Katika
ripoti hiyo hakuna mahali ilipoonesha nchi ilikuwa na hali mbaya ya
fedha na kwamba kwa kudhihirisha hilo, vigezo vya kimataifa vilionesha
bayana kuwa Deni la Taifa ni himilivu na nchi bado inakopesheka na
imeendelea kulipa mishahara watumishi wake pamoja na madeni mengine bila
kutetereka.
Alisema
Serikali iliendelea kulipa madeni mengi na hakuna kilicholegalega, huku
ikiendelea pia kugharimia shughuli za mihimili yote, ikiwemo Bunge,
usalama wa nchi na kuendelea kulipa madai ya makandarasi na watoa huduma
wengine.
Alisema
Serikali ya Awamu ya Tano imerithi mambo mengi mazuri yaliyofanywa na
serikali za awamu zilizopita, ikiwemo uchumi imara, umeme uliosambazwa
maeneo mengi vijijini na miundombinu
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )