STAA wa filamu Bongo, Jack Pentezel na
mumewe Gardner Dibibi wamefanya dua maalum ya kujivunia kutimiza miaka
mitatu ya ndoa iliyopitia changamoto nyingi.
Akipiga stori na paparazi wetu, Gardner
huku akisapotiwa na mkewe alisema ni jambo la kumshukuru Mungu kuifikia
tarehe ambayo walifunga pingu za maisha (Machi 22) tangu waoane mwaka
2013, kwa kuwa ni mengi yanayoongelewa na changamoto zilikuwa nyingi.
“Sina budi kumshukuru Mungu, unajua ndoa
za mastaa kudumu ni vigumu, mtu anaweza kuona ni safari fupi ya ndoa
lakini tumekumbana na changamoto nyingi hadi kufika leo hii na kizuri
kila siku ndiyo kwanza tunazidi kupendana japo wengi wamekuwa wakiomba
ndoa yetu ivunjike, tumeamua kusoma dua Mungu azidi kuisimamia ndoa
yetu,” alisema Gardner
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )