Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Mwaka ya utendaji wa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutoka kwa
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Kamishna Valentino Mlowola Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hundi Kifani yenye thamani ya
Shilingi Bilioni Sita kutoka kwa Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson mara
baada ya Taasisi ya Bunge kutekeleza kwa vitendo kauli ya kubana
matumizi yasio na Tija ili fedha hizo zikanunulie madawati kwa ajili ya
wanafunzi.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akiitazama Hundi Kifani yenye thamani ya
Shilingi Bilioni Sita mara baada ya kukabidhiwa na Naibu Spika Dkt.
Tulia Ackson mara baada ya Bunge kutekeleza kwa vitendo kauli ya kubana
matumizi ili fedha hizo zikatumike kwa ajili ya ununuzi wa madawati kwa
ajili ya wanafunzi.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson kulia,
Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilillah pamoja na wafanyakazi wengine wa
Bunge wakiwa wameishika hundi Kifani hiyo yenye thamani ya Shilingi
Bilioni Sita. Rais Dkt. Magufuli ameipongeza Taasisi ya Bunge kutokana
na hatua hiyo ya kubana matumizi na kuamua fedha zao zitumike katika
kununulia madawati kwa ajili ya wanafunzi.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameishika Taarifa ya Mwaka ya utendaji
wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mara baada ya
kukabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Kamishna Valentino
Mlowola Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson
kabla ya kukabidhiwa hundi kifani yenye thamani ya Shilingi Bilioni
Sita.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika tukio hilo la upokeaji wa
Taarifa yaUtendaji wa TAKUKURU pamoja na upokeaji wa Hundi Kifani
kutoka Taasisi ya Bunge Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo katika Hotuba yake ambayo
pia alitengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ane Kilango Malecela
ambaye alikubali kutoa taarifa ambazo si sahihi kuwa Mkoa wa Shinyanga
hauna watumishi hewa, japo katika uhakiki uliofanyika mara baada ya
taarifa hiyo kumebainika kuwa kuna zaidi ya watumishi 45 ambao ni hewa.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Mhandisi John Kijazi pamoja na Waziri wa Ofisi ya Rais Tamisemi,
Utumishi na Utawala bora Angela Kairuki Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu
Kiongozi Mhandisi John Kijazi wapili kulia, Dkt. Tulia Ackson wakwaza
kulia, Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilillah wakwanza kushoto,
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna Valentino Mlowola Ikulu Jijini Dar
es Salaam.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Mhandisi John Kijazi Taarifa ya Mwaka ya utendaji kazi wa Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Ikulu jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya Viongozi wa juu wa Jeshi la Magereza pamoja na Jeshi la Kujenga
Taifa JKT wakisikiliza kwa makini maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyokuwa akiyatoa Ikulu
jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )