Featured
Loading...

Tarehe ya Kikomo cha Daladala Zinazofanya Safari zake Katikati ya Jiji Dar es Salaam Yatajwa..Watakiwa Kubadilisha Ruti Kupisha Dart

 
Daladala zinazofanya safari zake katikati ya jiji zimetakiwa  kuondoka   ifikapo Mei
Hayo yameelezwa leo na Msemaji wa Mradi wa Mabasi  yaendayo kasi (Dart),  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Mkoa wa Dar  es Salaam (Darcoboa), Sabri Mabrouk. Amelisema tayari wamiliki wote wa mabasi walishalipwa fidia ya kubadili njia.

“Wamiliki wote wa mabasi wameshalipwa fedha zao tangu Desemba mwaka jana, hakuna anayedai na tumewapa siku saba kuondoka barabara kabla ya Mei 10,” amesema Mabrouk.

Mradi wa Dart unatarajia kuanza rasmi Mei 10, mwaka huu na tayari mabasi hayo yameshaanza kufanya majaribio katika njia mbali mbali katikati ya jiji huku changamoto kubwa ikidaiwa na waendesha pikipiki, raia na daladala kupita kwenye njia hiyo ya mradi na kusababisha msongamano wa magari kitendo ambacho kinalazimu mabasi hayo nayo kujikuta yakikaa foleni.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top