Bunge la Uingereza May 4
ilikuwa kama kuna vichekesho baada ya mjadala kuzuka ndani ya bunge
hilo kutokana na mmoja kati ya wabunge kuuliza swali kwa waziri mkuu wa
Uingereza, wakati wa muda wa maswali na majibu kuhusu mtangazaji wa BBC Gary Lineker kutotimiza ahadi yake.
Gary Lineker
Gary Lineker aliwahi kuhaidi kuwa kama Leicester City itafanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu Uingereza, basi atafanya TV show yake akiwa na nguo ya ndani pekee, kitendo ambacho bado hajakitekeleza, mbunge Keith Vaz ambaye ni shabiki mkubwa wa Leicester aliingia bungeni na Scarf ya Leicester na wakati wa maswali na majibu alimuuliza swali waziri mkuu wa Uingereza David Cameron.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )