Mshambuliaji aliuawa alipokuwa akikimbia baada ya kutekeleza tukio hilo
Mtu mmoja
aliyekuwa na Kisu na Shoka amewashambulia abiria waliokuwa kwenye Treni
Kusini mwa Ujerumani usiku wa jumatatu na kuwajeruhi watu wanne kabla
yeye kupigwa risasi na Polisi na kufa alipokuwa akikimbia baada ya tukio
hilo.
Polisi wa
mjini Wuerzburg wameeleza kwenye ukurasa wao wa Facebook kuwa abiria
watatu wamejeruhiwa vibaya na wengine 14 wanapata msaada wa kitabibu
kutokana mshtuko walioupata.
Polisi wamesema bado hakuna taarifa yeyote kuhusu sababu ya kutekelezwa kwa shambulio hilo.
vyombo
vya habari vya Ujerumani vimemnukuu msemaji wa wizara ya mambo ya ndani
mjini Bavaria kuwa mtu huyo ni mvulana wa miaka 17, mkimbizi mwenye
asili ya Afghanistan.
Mwaka
jana Ujerumani iliwaandikisha wahamiaji milioni moja waliokuwa wakiingia
nchini humo, zaidi ya 150,000 raia wa Afghanistan.
Tangu
mashambulizi ya hivi karibuni ya wanamgambo wa kiislamu nchini Ufaransa,
kumekuwa na hali ya hofu ya kutokea mashambulizi kama hayo nchini
Ujerumani, lakini mpaka sasa hakuna ishara zozote kuwa shambulio hilo
lilikua la kigaidi. BBC
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )