Babu Tale alisema haya kupitia kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio na kudai wasanii hao waliamua kuondoka chini ya uangalizi wake lakini kwa sasa wana maisha mabovu na yeye ana maisha mazuri.
“Unajua mtaa ndiyo uliwaambia wasanii waliondoka kwangu kuwa Babu Tale mwizi, na wakaaondoka Tip Top Connection lakini sasa hivi wasanii hao hao walioondoka kwangu wao wana maisha mabovu, wakati mimi na maisha mazuri. Wanakuja kwangu saizi wanataka niwasimamie kazi zao lakini mimi nasema sasa siwezi kwani wasanii nilio nao wananitosha” alisema Babu Tale.
Mbali na hilo Babu Tale alitoa ufafanuzi juu ya ukimya wa msanii Tunda Man na kusema kuwa wakati wake bado haujafika ila ukifika atarudi tu kwenye game na kudai kuwa saizi wana mpango wa kuachia ngoma nyingine ya Dogo Janja.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )