Waziri Simbachawene ameyasema hayo kwenye mahojiano maalumu na East Africa Radio kuhusu baadhi ya watendaji wa umma ambao wanamiliki kampuni ambazo zinashiriki kufanya tenda ya serikali na zimekuwa zikifanya vibaya na kusababisha malumbano baina ya wanachi na halmashauri mbalimbali nchini.
Amesema wamezuia swala hilo kisheria ili kuepuka usumbufu ambao umekuwa ukijirudia mara kwa mara pindi serikali ifanyapo ukaguzi wa utekelezaji wa kampuni hizo sambamba na kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu utendaji kazi wa kampuni hizo, ambazo zinakuwa zimepewa tenda na halmashauri mbalimbali nchini.
Amewataka wakurugenzi na viongozi wa mikoa kuzingatia sheria ya manunuzi inavyoelekeza na tayari wameanza uchunguzi kuwabaini watendaji wasio waaminifu juu ya swala hilo na pindi watakapogundulika kuhusika na swala hilo serikali itachukua hatua za kisheria.
Ametoa wito kwa watumishi wote wa serikali kutokujihusisha na swala hilo na wazingatie katika kusimamia haki na usawa kwa watanzania ambao ndiyo walipa kodi na watumiaji wa huduma mbalimbali za serikali.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )