Featured
Loading...

Cheka ajitupa kwenye ‘upromota’ wa ngumi, afungua kampuni yake ‘Cheka Promotion’

Baada ya kuwa nje ya ulingo kwa muda, bondia Francis Cheka ameamua kuwa promota wa ngumi na tayari amefungua Kampuni ya Cheka Promotion kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.
Bondia-Francis-Cheka
Cheka ambaye alikuwa bondia namba moja hapa nchini kwenye uzani wa super middle, amesema kwamba mbali na kuandaa mapambano, kampuni yake pia itakuwa ikiratibu na kusimamia mapambano atakayocheza mwenyewe.
“Leo (jana) ndipo tumekamilisha usajili wa Cheka Promotion, tunatarajia kuandaa pambano letu la kwanza Desemba ambalo litakuwa la Cosmas Cheka na bondia kutoka Uganda,” Cheka aliliambia gazeti la Mwananachi.
Cheka bingwa wa zamani wa WBC na WBO sanjari na yale ya Afrika ya UBO, IBF, WBO kabla ya kuvuliwa kutokana na kupatikana na kosa la kumpiga mtu nje ya ulingo na kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kabla ya kupunguziwa adhabu

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top