Featured
Loading...

Jibu la Zlatan kwa Cantona baada ya kuambiwa hawezi kuwa mfalme Man United


Jina la Eric Cantona sio geni masikioni mwa mashabiki wa soka ulimwenguni hususani mashabiki wa Man United, Eric Cantona ni miongoni mwa wachezaji nguli wa Man United ambao wamejijengea heshima kubwa Man United kutokana na umahiri wao katika uwanja enzi zao.
Cantona ambaye anatajwa au anajiita kama mfalme wa Man United alinukuliwa na Eurosport akisema kuwa yeye ndio mfalme pekee wa Man United, hawezi kutokea mwingine na kama akitokea mwingine basi hawezi kuwa mfalme atakuwa mtoto wa mfalme kauli ambayo ilimlenga moja kwa moja mshambuliaji mpya wa Man United Zlatan Ibrahimovic.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top