Featured
Loading...

Mshikaji wake Samatta alivyotua Leicester City na kumzungumzia Jamie Vardy


Mashabiki wa klabu ya Leicester wengi wangependa kusikia habari za mshambuliaji wao Jamie Vardy anasalia kikosini na kuendelea kukitumikia kikosi chao kwa msimu ujao, Ahmed Musa ambaye anacheza safu ya ushambuliaji amekiri kutamani kucheza pamoja na Vardy katika kikosi kimoja kutokana na aina yake ya uchezaji.
Musa ambaye ana umri wa miaka 23 alijiunga na Leicester City kwa dau la pound milioni 18 akitokea CSKA Moscow na kusaini mkataba wa miaka minne, “nafikiria mimi ni sawa na Jamie Vardy nina kasi na nacheza kwa bidii nafikiri tunafanana kwa vitu vingi, bado hatujawahi kucheza pamoja lakini nafikiria tutafit tukicheza pamoja”
3635801200000578-3695193-image-a-36_1468824455408
Mbwana Samatta aliwahi kukiri kuwa na urafiki na Ahmed Musa, baada ya mchezo kati ya Taifa Stars dhidi ya Nigeria uliochezwa September 5 2015 uwanja wa Taifa na kumalizika kwa suluhu, baada ya mchezo walibadilishana jezi na Samatta kusema Musa alimsaidia alipokuwa katika majaribio CSKA Moscow kutokana na yeye kutokujua lugha ya kirusi,

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top