Kampuni hii ya Klobaa iliundwa Mwaka 2015 huko US na sasa tunayofuraha kuwa imesajiliwa kufanya biashara hapa Tanzania pia..
Dhumuni letu kubwa ni kuwakutanisha wapenda starehe , watalii pamoja na watu wa kawaida sehemu moja ambayo watafurahia kwa pamoja na kuondoka wakiwa wameridhika na huduma, Sehemu hizo ni kama Club za usiku, Lounges, Baa, Migahawa, matamasha na vivutio vya utalii
Kwahiyo tunaweza sema Klobaa si tu ni Application ya simu lakini ni mtindo wa maisha ya kila siku
Klobaa App Kwa mara ya Kwanza inazinduliwa Tanzania Kesho Tarehe 30 July 2016 Hapa Dar es salaam Viwanja vya Posta Sayansi, Uzinduzi huo utaambatana na Tamasha Kubwa la Music Ambalo litahusisha wasanii Wakubwa hapa Tanzania na Kenya Wakiwemo Navy Kenzo , Ali Kiba , Sauti Soul , Christian Bella na Wengine Wengi
Kama wote mlivyosikia Tamasha Hilo ambalo limepewa Jina la "MWENDO KASI Festival" litakuwa la kwanza Africa lakini tutaendelea kufanya matamasha mbali mbali East Africa na Kwinginepo Afrika ili kuunganisha utamaduni wa kiafrika , Utalii na burudani
Kama njia ya Kurudisha Kwa jamii Klobaa miezi kadhaa ijayo inampango wakutoa Misaada kwa Vijana Kwa Kuwalipia ada baadhi ya Vijana waweze kusoma Elimu ya Juu hasa wale wasio na uwezo wa kujisomesha
Pia Tutakuwa tukifanya matamasha mbali mbali ya kuinua vipaji kwa wasanii na kuwasaidia kufanya kazi zao kupitia njia sahihi zitakazo wafikisha mbali zaidi...
Tunayofurahi Kuwatangazia Watanzania kuwa tumeamua Kuwachukua Kundi la mziki la Navy Kenzo Linaloundwa na Aika Marealle na Nahreel Kuwa wawakilishi wa Application ya KLOBAA Tanzania, Tumekuwa tukiwafatilia Navy Kenzo kwa muda mrefu na tumefurahishwa na maendeleo yao kimuziki kila siku zinavyoenda , Navy Kenzo Ambao kwa sasa wanamiliki Lebo ya Muziki ya The Industry wameonyesha mwamko mkubwa katika kukuza muziki wa Tanzania hivyo kufanya nao kazi imekuwa furaha yetu kubwa kwa kuwa tutafanya kazi na watu wanaojielewa katika ulimwengu wa burudani
Tunatumaini Huu ushirikiano kati ya Navy Kenzo na KLOBAA utatujenga wote kwa pamoja katika kutoa huduma nzuri kwa jamii Kwa ujumla hapa Tanzania na Kwinginepo Afrika....
Mwisho Kabisa Tunawakaribisha Kesho Kuja Kufurahi na sisi katika tamasha la Muziki la Mwendo Kasi Festival litakalofanyika Viwanja vya posta Kijitonyama kuanzia saa nane Mchana....
Wasanii Watakao Kuwepo Kwenye Tamasha hilo ni :
Navy Kenzo
Juma Nature
Ali Kiba
Sauti Soul
Manfongo
Christian Bella
Mr Blue
Isha Mashauzi
Roma
Nay wa Mitego
Joh Makini
G Nako
Nuh Mziwanda
Quick Rocka
Ruck Beiby
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )