Siku ya Ijumaa Chris Brown aliachia ngoma yake mpya yenye jina kama hilo ‘Shabba’ ndani ya wimbo huo akimshirikisha Wizkid na rapper wengine wachanga, Hoody Baby & Section Boyz.
Hata hivyo inadaiwa kuwa wimbo wa ‘shabba’ wa Wizkid ndiyo original japo umechelewa kutoka lakini Chris Brown ndiyo aliufanyia version wimbo huo kwa kumshirikisha Wizkid.
Nyota ya Wizkid imeonekana kuendelea kung’aa ndani ya Marekani kwa kufanya ngoma na mastaa wakubwa kadhaa huku wimbo wa ‘One Dance’ alioshirikishwa na Drake ukiendelea kufanya vizuri kwenye chati za Billboard na kumtambulisha vizuri msanii huyo wa Nigeria.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )