Baada ya Said Fella kutoa sababu za Ruby kutokuonekana kwenye video ya Yamoto Band kwa sababu zinazodaiwa kuwa ni stress, Ruby nae amefunguka.
Rubby
amesema Yamoto Band hawakuona umuhimu wake kwenye video hiyo ndiyo
maana waliweza kushoot video hiyo siku ambayo yeye alikuwa busy na mambo
yake mengine.
“Unajua
siku ambayo wao walikuwa wakishoot video hiyo mimi nilikuwa na mambo
yangu mengine hivyo nilikuwa busy, niliwaomba kama wanaweza wanisubiri
kidogo nimalizane na hizo kazi zangu lakini wao wakafanya video hiyo,
hilo linatosha kuonyesha sikuwa na umuhimu.” alisema Rubby
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )