Featured
Loading...

Serikali imeyafutia usajili magazeti 473


Serikali imefuta usajili wa magazeti 473 ambayo hayajachapishwa kwa kipindi cha miaka mitatu.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo,  Nape Nnaye
Hatua hiyo imetangazwa leo na Waziri wa Habari, Nape Nnauye katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Ukumbi wa Maelezo.
Amesema mtu yeyote atakayechapisha magazeti hayo kwa njia ya nakala ngumu (Hard copy) au kielektroniki atachukuliwa hatua za kisheria.
“Iwapo kuna mmiliki wa gazeti ambaye angependa kuendelea na biashara hii milango iko wazi kwa ajili ya kuwasilisha maombi mapya sio kuuhuisha yaliyofutwa,” alisema Nape.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top