Aliyekuwa mke wa Mr Flavour, Anna Banner amesaini dili ya kuwa balozi na kampuni ya vipodozi – VEEBEEZ.
Baada ya kusaini dili hilo na kampuni hiyo, Anna Banner kupitia akaunti yake ya instagram aliandika, “MEET THE NEW BRAND AMBASSADOR OF VEEBEEZ (THE VALERIE BRAND).”
Anna Banner ni muigizaji wa filamu nchini Nigeria aliyetengana na staa huyo wa muziki wa Nigeria, Mr Flavour mapema mwezi Juni mwaka huu huku wakiwa wamebahatika kupata mtoto mmoja [Sophia Okoli] kwenye mahusiano yao.
Picha ya Anna Banner akisaini mkataba
Anna Banner alifanikiwa kushiriki kwenye mashindano ya kumtafuta Miss Nigeria mwaka 2013 lakini pia aliwahi kushinda kwenye shindalo alilochaguliwa kama msichana mzuri zaidi nchini Nigeria. Hilo ni dili la kwanza la ubalozi alilolipata Banner.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )