Picha ya kwanza iliyotumwa na Juno
Picha hiyo iliyotolewa na NASA Jumanne hii inaonesha sayari hiyo ikiwa imezungukwa na miezi mitatu kati ya miezi yake minne mikubwa.
Miezi inayoonekana ni Lo, Europa na Ganymede. Mwezi huo mwingine uitwao Callisto hauonekani.
Picha hiyo ilipigwa Jumamosi wakati Juno ilipokuwa inazunguka sayari hiyo ikiwa umbali wa maili milioni tatu.
Hata katika umbali huo, Shimo Jekundu, lililosababishwa na dhoruba kali kwenye sayari hiyo karne nyingi zilizopita, linaonekana.
Juno iliingia katika mzingo wa Jupiter wiki iliyopita na kuanza kuizunguka sayari hiyo ambalo pia hufahamika kama Zohali au Zozali.
Safari yake kutoka duniani hadi ilichukua miaka mitano.
Juno itachunguza na kupeleleza sayari hiyo kwa miezi 20, lengo kuu likiwa kusaidia wanasayansi kubaini asili ya sayari hiyo ambayo wanaamini inaweza kuwasaidia kuelewa zaidi asili ya mfumo wa jua.
Chombo hicho cha juu kilipokuwa kinaikaribia Jupiter, kamera zake na mitambo mingine muhimu vilizimwa kuzuia visiharibiwe na miali nururishi. Baadaye, vilifunguliwa.
Wanasayansi wanatarajia picha za karibu zaidi za Jupiter zitapokelewa mwezi ujao.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )