Featured
Loading...

Wapinzani wa Yanga kuwasili Alhamisi hii


Wapinzani wengine wa klabu ya Yanga, katika michuano ya kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika, timu ya mpira wa miguu ya Medeama kutoka Ghana, itawasili Dar es Salaam, Alhamisi hii.
CAF (1)
Yanga itaikaribisha Medeama ikiwa ni mchezo wa tatu kuwania taji hilo hatua ya makundi. Mchezo huo utafanyika saa 10 jioni kwneye uwanja wa taifa, July 16.
Huu ni mchezo wa tatu kwa Yanga katika harakati za kuwania kombe la shirikisho hatua ya makundi. Michezo miwili ya awali ilikuwa ni dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria ambako ilipoteza kwa bao 1-0 kabla ya kupoteza tena dhidi ya TP Mazembe, mechi iliyopigwa jijini Dar es Salaam.
Mchezo wa Jumamosi utachezeshwa na waamuzi kutoka Misri ambao ni Ibrahim Nour El Din atakayekuwa mwamuzi wa kati; akisaidiwa na Ayman Degaish na Samir Gamal Saad wakati mwamuzi wa akiba akiwa ni Mohamed Maarouf Eid Mansour.
Kamishna wa mchezo huo atakuwa Pasipononga Liwewe kutoka Zambia na maofisa wasimamizi ni Mfubusa Bernard ambaye atasimamia utendaji wa waamuzi wakati Mratibu Mkuu wa mchezo huo kutoka CAF atakuwa Ian Peter Keith Mc Leod.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top