Klabu ya Mbeya City ya jijini Mbeya kwa sasa imeweka kambi Matema Beach Kyela Mbeya kwa muda kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu soka Tanzania bara, Mbeya City ambayo inafundishwa na kocha kutoka Malawi Kinnah Phiri, imeweka wazi baadhi ya taarifa zake kuhusu usajili.
Mbeya City kupitia afisa habari wake Dismas Ten imethibitisha kukamilisha usajili wa Mohamed Mkopi na Rajab Zahir hadi sasa, Kwa upande wa golikipa Juma Kaseja ambaye wengi tunafahamu kuwa kamaliza mkataba na Mbeya City, vipi mipango ya klabu imeachana nae jumla au tutaendelea kumuona akiidakia Mbeya City msimu ujao?
“Kuhusiana
na usajili hadi sasa Mbeya City imefanikiwa kusajili wachezaji wawili
Mkopi na Rajab Zahir, kuhusu mapendekezo gani mwalimu kapendekeza katika
usajili hiyo inabakia kuwa siri kwa uongozi, ni kweli Kaseja kamaliza
mkataba na Mbeya City na bado mapema siwezi kusema kama tutakuwa nae
msimu ujao au la”
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )