MAELEZO YA KAIMU MKURUGENZI MKUU, MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA, ENG. JAMES KILABA KUHUSU UAMUZI KUHUSU UKIUKWAJI WA MASHARTI YA USAJILI WA NAMBA/LAINI ZA SIMU ZA MKONONI
Ndugu Waandishi wa Habari,
Tumewaita
hapa leo ili kutoa uamuzi kuhusu mashauri ya ukiukwaji wa masharti ya
usajili wa namba/laini za simu za mkononi uliofanywa na makampuni ya
simu za mkononi.
Makampuni hayo ni:
1. Airtel Tanzania Limited,
2. Benson Informatics Limited ambayo inatumia jina la biashara la SMART,
3. MIC Tanzania Limited ambayo inatumia jina la biashara la TIGO,
4. Viettel Tanzania Limited ambayo inatumia jina la biashara la Halotel,
5. Vodacom Tanzania Limited,
6. Zanzibar Telecom Limited ambayo inatumia jina la biashara la Zantel.
Makampuni
hayo yamekiuka masharti ya usajili wa laini na matumizi ya laini kama
yalivyoaninishwa kwenye Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta
(EPOCA) ya 2010 na Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za
Leseni za 2011.
Kabla
ya kuelezea uamuzi huo, naomba kwanza nitoe maelezo ya awali kuhusiana
na suala zima la usajili wa laini/namba za simu za mkononi.
Itakumbukwa
kwamba usajili wa namba simu umekuwa ni wa lazima baada ya sheria ya
EPOCA ya 2010 kuanza kutumika. Kifungu cha 102(1) cha EPOCA kinafafanua
kwamba mtu yeyote ambaye anamiliki simu ya mkononi ana jukumu la kutoa
taarifa kwa mtoa huduma ikiwa kutakuwepo na mabadiliko ya umiliki wa
simu hiyo au namba iliyosajiliwa kwa jina lake. Kifungu 102 (2)
kinamtaka yeyote ambaye atataka kutumia simu au namba ambayo ilikuwa
inatumiwa na mtu mwingine kusajili simu na namba hiyo. Aidha Kanuni za
Watumiaji (The Electronic and Postal Communications (Consumer
Protection) Regulations 2011) na Kanuni za leseni (Licensing Regulations
2011) zina vipengele kuhusu usajili wa namba za simu.
Kanuni
ya 10(2) ya Kanuni za watumiaji kinasema mtu yeyote ambaye anamiliki au
ana nia ya kutumia laini ya simu au kifaa chenye laini ya simu ndani
anatakiwa kujisajili kwa mtoa huduma au wakala aliyeidhinishwa.
Kanuni
ya 33(1) ya Kanuni za leseni kinaeleza kwamba mtu yeyote ambaye anauza
au kwa namna yeyote ile anatoa laini ya simu au kifaa chenye laini ya
simu ndani anatakiwa kuandikisha wateja kwa kutumia fomu maalum ambayo
inamtaka mtumiaji atoe kitambulisho chenye picha yake halisi.
Sababu za kuanzisha utaratibu wa kusajili namba za simu ni pamoja na:-
(i) Kuwalinda watumiaji na jamii kutokana na matumizi mabaya ya huduma za mawasiliano.
(ii)
Kuwezesha kuwatambua watumiaji wa huduma za ziada za simu, kama huduma
za kibenki, kutuma na kupokea fedha, kufanya malipo mbalimbali kwa
kutumia simu kwa mfano kulipia huduma za maji, umeme, vipindi vya
televisheni vya kulipia n.k.
(iii) Kuimarisha usalama wa taifa.
(iiii) Kuwawezesha watoa huduma za mawasiliano kuwafahamu vizuri wateja wao na kuwahudumia ipasavyo kadri ya mahitaji yao.
(v) Kuwa na taarifa za matumizi ya simu za mkononi kwa ajili ya mipango ya maendeleo ya sekta.
Mnamo
Aprili 2013 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na makampuni yanayotoa
huduma za simu za mkononi walikubaliana juu ya hatua za kumaliza kasoro
zilizokuwa zimejitokeza katika usajili wa namba za simu. Aidha
walikubaliana kutokuwezesha laini/namba za simu kutumika kabla ya
usajili kukamilika na taarifa za mteja kuhakikiwa.
Makubaliano mengine yalikuwa kwamba mitandao ya simu isifanye kile kinachoitwa ‘ usajili wa awali’.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inafanya ukaguzi wa mara kwa mara wa usajili wa namba za simu.
Hivi
karibuni, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imekagua mifumo ya usajili wa
laini za simu na kugundua ukiukwaji katika maeneo manne:
1. Namba kutolewa bila mteja kutakiwa kusajiliwa.
2. Namba kusajiliwa kwa majina, vitambulisho na nyaraka za watu wengine.
3. Namba kutokufungwa hadi usajili ukamilike
4. Namba kusajiliwa usajili wa awali.
Makampuni sita ambayo yaligunduliwa kutenda makosa hayo yote au baadhi yaliitwa na MamKatulanda Fred1:
laka
ya Mawasiliano Tanzania tarehe 2 na 3 Juni 2016 na kutakiwa kutoa
utetezi wao kuhusu ukikwaji wa masharti ya Usajili wa namba za simu za
mkononi.
Kufuatia
kusikilizwa kwa mashauri hayo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ilifikia
uamuzi ufuatao kwa kila kampuni ya simu za mkononi husika:
UAMUZI:
Baada
ya kusikiliza utetezi wa Mtoa Huduma kwa maelezo ya mdomo na maandishi,
na baada ya kuzingatia utetezi huo, ni wazi kwamba Mtoa Huduma amekiuka
kanuni ya 33 ya Kanuni za Leseni za mwaka 2011 zilizotolewa chini ya
Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) na pia amekiuka
vifungu 93,130 na 131 vya Sheria hiyo.
Kwa
kuzingatia kwamba ni wajibu wa Mtoa Huduma kuhakikisha kwamba uuzwaji
na utoaji wa laimi za simu unafanyika kwa mujibu wa kifungu 93 (2,3 na
4) cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya 2010, na
Kanuni ya 33 ya Kanuni za Leseni za 2011 na kwamba Mtoa Huduma amekiuka
matakwa ya Sheria; na
KWA
KUTAMBUA KWAMBA matumizi mabaya ya laini/ namba za simu za mkononi
kunahatarisha usalama wa Taifa na kunachochea tabia hatarishi katika
jamii na kunaendeleza tabia za kiuhalifu nchini;
KWA HIYO BASI, Mamlaka inatoa AMRI kama ifuatavyo:
1. AIRTEL TANZANIA LIMITED ilipe kwa Mamlaka,ifikapo 30 Julai 2016 faini kama ilivyoainishwa hapa:
(a)
SHILINGI 74,000,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Sabini na Nne) kwa
kuruhusu kuuzwa kwa laini 148 bila kutumia kitambulisho halisi cha
mnunuzi.
(b)
SHILINGI 33,500,000 (shilingi za Kitanzania Milioni thelathini na tatu
na laki tano) kwa kuruhusu laini 67 ziuzwe bila kujaza fomu ya usajili.
(c)
SHILINGI 32,500,000 (shilingi za Kitanzania Milioni thelathini na mbili
na laki tano) kwa kuruhusu laini 65 ziwashwe kabla ya kuuzwa; na
(d)
SHILINGI 42,500,000 (shilingi za Kitanzania Milioni arobaini na mbili
na laki tano) kwa kuruhusu laini 85 zifanyiwe usajili wa awali na
kutumika kwenye mtandao wake.
2. BENSON INFORMATICS LIMITED ilipe kwa Mamlaka,ifikapo 30 Julai 2016 faini kama ilivyoainishwa hapa:
(a)
SHILINGI 7,000,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Saba) kwa kuruhusu
kuuzwa kwa laini 14 bila kutumia kitambulisho halisi cha mnunuzi.
(b) SHILINGI 7,000,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Saba) kwa kuruhusu laini 14 ziuzwe bila kujaza fomu ya usajili; na
(c) SHILINGI 3,000,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Tatu) kwa kuruhusu laini 6 ziwashwe kabla ya kuuzwa.
3. MIC TANZANIA LIMITED ilipe kwa Mamlaka,ifikapo 30 Julai 2016 faini kama ilivyoainishwa hapa:
(a)
SHILINGI 93,500,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Tisini na Tatu na
Laki Tano) kwa kuruhusu kuuzwa kwa laini 187 bila kutumia kitambulisho
halisi cha mnunuzi;
(b)
SHILINGI 43,500,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Arobainii na tatu
na laki tano) kwa kuruhusu laini 87 ziuzwe bila kujaza fomu ya usajili;
(c) SHILINGI 41,000,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Arobaini na Moja) kwa kuruhusu laini 82 ziwashwe kabla ya kuuzwa; na
(d)
SHILINGI 11,000,000 (shilingi za Milioni Kumi na Moja) kwa kuruhusu
laini 22 zifanyiwe usajili wa awali na kutumika kwenye mtandao wake.
4. VIETTEL TANZANIA LIMITED ilipe kwa Mamlaka,ifikapo 30 Julai 2016 faini kama ilivyoainishwa hapa:
(a)
SHILINGI 36,500,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Thelathini na sita
Laki Tano) kwa kuruhusu kuuzwa kwa laini 73 bila kutumia kitambulisho
halisi cha mnunuzi.
(b)
SHILINGI 36,000,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Thelathini ba Sita)
kwa kuruhusu laini 72 ziuzwe bila kujaza fomu ya usajili; na
(c)
SHILINGI 34,500,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Thelathini na Nne
Laki Tano) kwa kuruhusu laini 69 ziwashwe kabla ya kuuzwa.
5. VODACOM TANZANIA LIMITED ilipe kwa Mamlaka,ifikapo 30 Julai 2016 faini kama ilivyoainishwa hapa:
(a)
SHILINGI 49,000,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Arobaini na Tisa)
kwa kuruhusu kuuzwa kwa laini 98 bila kutumia kitambulisho halisi cha
mnunuzi;
(b)
SHILINGI 24,000,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Ishirini na Nne)
kwa kuruhusu laini 48 ziuzwe bila kujaza fomu ya usajili;
(c) SHILINGI 19,000,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Kumi na Tisa) kwaKatulanda Fred1:
kuruhusu laini 38 ziwashwe kabla ya kuuzwa; na
(d)
SHILINGI 4,500,000 (shilingi za Milioni Nne na Laki Tano) kwa kuruhusu
laini 9 zifanyiwe usajili wa awali na kutumika kwenye mtandao wake.
6. ZANZIBAR TELECOM LIMITED ilipe kwa Mamlaka,ifikapo 30 Julai 2016 faini kama ilivyoainishwa hapa:
(a)
SHILINGI 36,500,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Thelathini na sita
na Laki Tano) kwa kuruhusu kuuzwa kwa laini 73 bila kutumia kitambulisho
halisi cha mnunuzi;
(b)
SHILINGI 11,500,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Kumi na Moja na
Laki Tano) kwa kuruhusu laini 23 ziuzwe bila kujaza fomu ya usajili;
(c) SHILINGI 7,000,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Saba) kwa kuruhusu laini 14 ziwashwe kabla ya kuuzwa; na
(d)
SHILINGI 2,000,000 (shilingi za Milioni Mbili) kwa kuruhusu laini 4
zifanyiwe usajili wa awali na kutumika kwenye mtandao wake.
Pamoja na faini hizi, Watoa huduma hawa wametakiwa kuchukua hatua zifuatazo:
a)
Kuwasilisha Mamlaka a Mawasiliano Tanzania ifikapo 15 Julai 2016 orodha
iliyohakikiwa ya wakala wa kusambaza na kuuza laini za simu nchi nzima
kama inavyotakiwa na kifungu 92(2) cha EPOCA;
b) Kuacha mara moja kuwatumia wakala au wasambazaji wasioruhusiwa kuuza au kusambaza laini za simu nchini;
c)
Kuhakikisha kwamba laini za simu zinauzwa na Wakala anayetambuliwa na
Mtoa Huduma na ambaye ana anwani ya makazi inayofikika na pia mwenye
Namba Tambulishi ya Mlipa Kodi (Tax Payer Identification Number); na
d)
Kuzima laini zote zilizo sokoni ambazo zimewashwa na kuwasilisha
taarifa ya utelekezaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ndani ya siku
saba kutoka tarehe walizopokea Uamuzi huu.
Mtoa
Huduma yoyote atakayekaidi utekelezaji wa AMRI atachukuliwa hatua kali
za kisheria ikiwa ni pamoja na kushtakiwa kwa makosa ya jinai.
Mwisho, napenda kumalizia uwasilishaji wa uamuzi huu kwa kusisitiza yafuatayo:
Utaratibu
wa kusajili laini za simu za mkononi unawahusu watoa huduma na
watumiaji pia. Watumiaji, watoa huduma, wakala wa makampuni ya simu za
mkononi na wananchi kwa ujumla wanakumbushwa kwamba ni kosa kisheria
kutumia au kuwezesha kutumiwa kwa namba ya simu ambayo haikusajiliwa.
Ni
kosa la jinai kutumia namba ya simu isiyosajiliwa. Adhabu ni faini ya
shilingi laki Tano au kifungo cha miezi mitatu. Kusajili nenda kwa mtoa
huduma wako au wakala wake ukiwa na kitambulisho chenye picha yako. Toa
taarifa sahihi.
Aidha ni kosa kusajili laini kwa kutumia majina yasiyo sahihi.
Watumiaji wote ambao hawasajili namba zao za simu wafanye hivyo mara moja. Kuthibitisha usajili wako piga *106#.
Asanteni kwa kunisikiliza.
IMETOLEWA NA:
KAIMU MKURUGENZI MKUU,
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
4 JULAI, 2016
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )