Kila siku
asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti
ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya
Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza
kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya yalioandikwa ni huu utafiti wenye kwenye gazeti la Mtanzania yenye kichwa ‘Uhusiano wa kula matunda na furaha’
Ulaji wa matunda na mboga za majani unaweza kukusaidia kupata furaha, utafiti mmoja wa Australia umegundua. Watafiti
hao wamegundua kuwa watu waliobadili mtindo wao wa ulaji, na kuanza
kula matunda na mboga za majani kwa wingi katika mlo wao wa kila siku
wamepatwa na ongezeko la kuwa na hisia za furaha na kuridhikaa kimaisha
ikilinganishwa na namna ile ile ambayo mtu asiye na ajira anavyohisi
mara apatapo ajira limeeleza jarida ‘la American Journal of Public
Health.
Redzo
Mujcic ambaye ni mtafiti mwenza wa afya na uchumi katika chuo kikuu cha
Queensland nchini Australia amesema……..>>>”Ni
wazi kuwa ulaji wa matunda na mboga za majani huongeza furaha yetu kwa
kasi zaidi kuliko inavyoongezeka kutokana na afya ya muhusika’‘
Utafiti
uliofanyika kabla ya huo ulionyesha kwamba kula mboga na matunda mengi
kumesaidia mno kuimarisha sana afya ya miili ya watu, lakini faida kama
hizo zinaanza kuonekana baada ya kipindi kirefu cha wakati, wamesema
watafiti hao.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )