Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amemtangaza
Bw.Hassan Abbas kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji
Mkuu wa Serikali kuanzia Agosti 5 Mwaka huu.
Uteuzi
huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria za Utumishi wa Umma Namba 8 ya
mwaka 2002 kifungu Namba 6(1)(b) kufuatia uhamisho wa aliyekuwa
Mkurugenzi wa Idara hiyo Bw. Assah Mwambene uliofanyika tarehe 7 Machi
2016 kwenda Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mhe.Nape
Moses Nnauye ametoa wito kwa Wanahabari na Wananchi kwa ujumla kutoa
ushirikiano wa kutosha kwa Bw Abbas atakapokuwa anatekeleza majukumu
yake.
“Ninawaomba
Wanahabari na Watanzania kwa ujumla mumtambue Bw Abbas na mtoe
ushirikiano unaostahili katika utendaji wa kazi zake”.Alisema Mhe. Waziri.
Aidha
Mhe. Waziri Nape alimpongeza Bibi Zamaradi Kawawa aliyekuwa anakaimu
nafasi hiyo kwa kujituma na kusimamia majukumu yote ya Idara kwa
ukamilifu na uadilifu.
Kwa
upande wake Mkurugenzi huyo mpya amekubali uteuzi huo na ameahidi
kuitumikia nafasi hiyo kwa uadilifu mkubwa na ameomba ushirikiano wa
kutosha kutoka kwa wafanyakazi wa Idara ya Habari Maelezo na Watanzania
kwa ujumla.
Kabla
ya uteuzi huo Bw. Hassan Abbas alikuwa ni Meneja Habari na Mawasiliano
katika Ofisi ya Rais inayosimamia Utekelezaji wa Program ya Matokeo
Makubwa sasa (President`s Delivery Bureau).
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )