Chama
cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Serikali kumpiga marufuku Katibu Mkuu wa
Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad kuhudhuria hafla na
matukio ya kitaifa kutokana na kitendo alichokifanya hivi karibuni
kwenye msiba wa Rais wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Aboud
Jumbe.
Maalim
Seif alikataa kumpa mkono Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein
kufuatia msimamo wa chama hicho wa kutoshirikiana na Serikali Visiwani
humo, wakipinga kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 na
Kufanyika kwa Uchaguzi wa Marudio uliompa ushindi wa kishindo Dkt. Shein
baada ya CUF kuususia.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai alisema kuwa ni muda
muafaka sasa kwa Serikali kumzuia kushiriki matukio ya kitaifa. Alisema
CCM imefadhaishwa na kitendo alichokifanya Maalim Seif na kuwataka watu
wote kukilaani.
“Nawaomba
watu wasiendekeze sakata hili kwa sababu linamdhalilisha Maalim,”
alisema Vuai. “Hatukutarajia kiongozi kama Maalim kufanya kitendo kama
kile,” aliongeza.
Hili
ni tukio la kwana kwa Maalim kugoma kumsalimia Dkt. Shein. Awali, Dkt.
Shein alimtembelea Maalim Seif na kumjulia hali katika hotel ya Serena
jijini Dar es Salaam na walizungumza vizuri wakiombeana heri.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )