Diamond Platnumz na Alikiba watachuana mwaka huu kuwania kipengele cha
Best Male Eastern Africa kwenye tuzo za All Africa Music [Awards] 2016
za nchini Nigeria.
Waandaji
wa tuzo hizo wametoa orodha ya kwanza ya wasanii wanaowania mwaka
huu.Diamond na Kiba wana upinzani pia kutoka kwa Bebe Cool, Eddy Kenzo,
Jose
Chameleone na Navio wa Uganda.
Hata hivyo hakuna msanii wa Tanzania
aliyetajwa kwenye kipengele hicho upande wa wanawake.Tuzo hizo zitatolewa mwezi November jijini Lagos, Nigeria.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )