Featured
Loading...

FBI akiri kuwa jasusi wa Uchina


 Mfanyikazi mmoja wa shirika la kijasusi la Marekani FBI amekiri mbele ya mahakama ya nchini humo kwamba yeye alikuwa jasusi wa serikali ya Uchina.

Kun Shan Chun, ambae alizaliwa Uchina lakini ana uraia wa Marekani akiitwa Joey ,alikiri hatia ya kupeleka habari za siri kwa maafisa wa serikali ya Uchina.

Mwanasheria wa Marekani Preet Bharara amesema Joey yaani Kun Shan Chun amehatarisha usalama wa nchi kwa njia hiyo ya usaliti wa hali ya juu.

Kupitia wakili wake , Chun amejitetea akasema anajutia kitendo hicho na kwamba anaipenda Marekani .
Hata hivyo upande wa mwendesha mashtaka na vilevile upande wa utetezi umekubaliana kuwa anastahili adhabu ya hata zaidi ya miaka 21 jela.

Ubalozi wa Uchina mjini Washington bado haujatoa tamko lolote kufikia wakati wa kuchapishwa kwa taarifa hiyo.

Chun, mwenye umri wa miaka 46,amekuwa akifanya kazi na FBI kama mhandisi wa mitambo ya kielectronic kutoka 1997 hadi alipokamatwa hapo mwezi March.

Alijuana na maafisa wa serikali ya UChina katika mojawapo ya ziara za kikazi huko Uitaliano na Ufaransa hapo 2011, na kisha akaendelea kukutana nao na kufanya nao kazi kisiri.

Alifunika zaidi siri hiyo kupitia kampuni ya kichina ya kitechnologia iitwayo Zhuhai Kolion,ambapo pia alinufaika kifedha.

Katika vitu ambavyo aliviwasilisha a kwa maafisa hao waChina ni chati iliyoonesha maafisa mbalimbali wa FBI na vyeo vyao na pia picha, na stakabadhi yenginezo za ziri.

Kwa habari hizo alizotoa alizawadia si tu fedha bali pia kulipiwa gharama za kwenda ziara za likizo mahakama imeelezwa hayo.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top