Msanii wa label ya WCB, Harmonize amefuta tattoo ya zamani ya Diamond na
amechora tattoo nyingine tatu mpya ikiwemo ya bosi wake huyo pamoja na
nyingine ya mama yake mzazi.
Mapema mwezi Januari mwaka huu msanii huyo aliamua kuchora tattoo ya
picha ya Diamond na chini yake aliandika jina la Simba ambalo anatumia
hitmaker huyo wa ‘Kidogo’ kwa kudai kuwa bosi wake huyo ametoa mchango
mkubwa sana kwenye maisha yake ya muziki ndio maana akaamua kufanya
hivyo.
Picha ya tattoo za Harmonize za zamani
Harmonize amepost picha kwenye mtandao wake wa Instagram inayomuonyesha
akiwa na michoro mipya kwenye mkono wake wa kulia akiwa amechora picha
ya Diamond, mama yake mzazi pamoja na picha nyingine ya dini la Almasi.
Picha ya tattoo mpya za Harmonize
“Mama Rajabu & Simba @wasafistudios,” ameandika Harmonize kwenye picha aliyoiweka kwenye mtandao huo.
Lakini baadhi ya mashabiki walio comment kwenye picha hiyo wamemtaka
msanii huyo achore na tattoo nyingine ya baba yake kwa kuwa kumuweka
mzazi mmoja pekee ni kama amefanya upendeleo.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )