Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Kulia) akiwaeleza jambo viongozi
wa CUF walioongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Mhe. Maalim Seif
Sharif Hamad (Katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Julius
Mtatiro waliomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo Agosti
13, 2016. Mhe. Spika, Job Ndugai amerejea nchini hivi karibuni akitokea
nchini India alikokwenda kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Kulia) akifurahia jambo na Katibu
Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (Katikati)
na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Julius Mtatiro waliomtembelea
nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo leo Agosti 13, 2016 .
Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Kulia) akimweleza jambo Katibu
Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (kushoto)
aliyeambatana na viongozi wenzake wa CUF nyumbani kwa Mhe. Spika Job
Ndugai leo leo Agosti 13, 2016 jijini Dar es salaam.
Naibu katibu mkuu wa CUF, Bara na
Mbunge wa Kaliua, Tabora Mhe. Magdalena Sakaya akimweleza jambo Mhe.
Spika, Job Ndugai (hayupo pichani) mara baada ya kumtembelea Mhe. Spika
leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF
Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )