Kadi ya kumtambulisha mtoto Happiness John (5) kimataifa baada ya
kufanyiwa upasuaji na kuwekewa betri ndani ya moyo inatengenezwa nchini
Afrika Kusini. Happiness ambaye alifanyiwa upasuaji huo Julai 15 na
kuruhusiwa kutoka hospitalini wiki moja iliyopita, anatakiwa kuwa na
kadi tambulishi ambayo itamuwezesha kutofanyiwa ukaguzi wa
kielektroniki. Kwa sasa mtoto huyo amepewa kadi ya muda ambayo
inamruhusu kutopita katika maeneo yenye mionzi kwa ajili ya ukaguzi,
ikiwamo viwanja vya ndege na majengo yenye ulinzi mkali.
Tuendelee kumtakia heri mtoto huyu
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )