Watu wengi miaka ya hivi karibuni wamekuwa wanaogopa sana uzee na
wengine wamejikuta hata wakikanusha kuwa wao si wazee hata pale
wanapoonekana tayari wameanza kuzeeka.
Leo ninazo hizi sababu ambazo zinaweza kukufanya kuzeeka kwa haraka zaidi
Mazoezi ni muhimu sana kwa mtu mtu yoyote kwani husaidia ngozi ya mwili
kuendelea kuwa vizuri. Hivyo ni vizuri kufanya mazoezi angalau dakika 20
kwa siku.
Kukosa usingizi.
Kwa kawaida binadamu anatakiwa apate muda wa kulala angalau saa 7 hadi 8 siku haijalishi yuko.
Uvutaji wa sigara
Sigara si nzuri kiafya na huchangia kuuchosha mwili mapema hivyo ni
vyema kama unatumia sigara ukaacha mara moja na kama unashindwa unaweza
kuwatafuta wataalam wakusaidie.
Acha kubeba visasi moyoni
Jifunze kusamehe watu ambao wamekukosea maishani, kwani unaposamehe
unaufanya moyo wako kuwa safi. Watu ambao wanabeba visasi na vinyongo
hupata makunyazi ya ngozi na kuzeeka haraka.
Kunywa pombe sana
Watumiaji wa vileo kwa wingi huwa katika hatari pia ya kuzeeka mapema
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )