Kuna urembo mbalimbali wa macho kulingana na taste ya mtu na mapendeleo yake . Leo nitazungumzia "smoky eyes" au macho yaliyapambwa kwa eye liner, mascara na eye shadows zenye rangi nyeusi, grey au za mng'aro.
Jinsi ya kuremba jicho:
-hakikisha uso na ngozi inayozunguka jicho ni safi kabla ya kuanza urembo wowote usishawishike kupaka vipodozi juu ya ngozi chafu haitakaa vizuri make up yako. Safisha kwa kutumia face towel iliyochovywa kwenye maji ya moto(huwa naona ni rahisi kwangu hasa kama kitambaa nitumiacho ni cheupe ni rahisi kujua kuwa u msafi au la kwa kuangalia kitambaa) kamwe usioshe uso wako kwa sabuni au maji ya moto. Ngozi ya uso iko rahisi kudhulika ikipata msukosuko kidogo. Sabuni huwa na kemikali nyingi na maji ya moto yanapausha uso. kama utalazimika kutumia sabuni osha uso kwa maji ya baridi kwa muda kiasi ili kuondoa kemikali zitakazokuwa zimeachwa.
- tayarisha kope/eye lids zako kwa kupaka wanja mweusi kwa uangalifu au eyeliner ya dark colour kama ni mtu anayejiamini unaweza tumia rangi yoyote ile sababu si wote wanaweza paka rangi ya njano au kijani na wakawa confident na muonekano wao.
-Kwa matokeo mazuri uwe na eye shadow za aina mbili moja ya rangi iliyokolea na nyingine iliyo light. Anza na rangi iliyo light paka kwa uangalifu kuelekea kona ya nyusi kama picha hapo chini
endelea kama unapenda ming'ao machoni(hususani kwa sherehe) unaweza kupaka juu ya kope zako ila hakikisha hufiki mbali sana karibu na nyusi . Kisha malizia na darker colour kama picha ya kulia inavyoonyesha anzia kona ya kushoto ya jicho kwenda kulia kwa kiasi upendacho.
-Linganisha macho yako yote kama yana muonekano sawa kisha unaweza kuongezea mascara kwa juu ya nyusi ikiwa ni mpenzi.
till next time..
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )