Featured
Loading...

WAHEREHEKEA MIAKA 100 YA NYWELE ZA KIAFRIKA


MIT
Zaidi ya watu mia mashuhuri walifika  katika kusherehekea ya miaka 100 ya nywele za Kiafrika, shughuli hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam tarehe 15 Agosti na Ulikuwa ni uzinduzi wa kipekee.
Yote ilikuwa ni kuhusu uwezeshaji wa mwanamke wa Kiafrika. kauli mbiu ya shughuli hii ilikuwa ni “Kila ndoto ni halali” Usiridhie
Darling Group, kama kiongozi wa soko la nywele  na biashara za huduma ya nywele Afrika , walitambulisha bidhaa zao mbalimbali za Aliyana professional kwa watengeneza nywele wote nchini Tanzania. Tukio hilo pia lilipambwa na wanamitindo mahili wa Tanzania   
Wakati maonesho ya mavazi yakiendelea, wageni walitambuliswa  mfululizo wa bidhaa za nywele  za  Aliyana Professional Shine na Aliyana Professional enrich zenye ubora wa hali ya juu katika kuimarisha nywele.
Wanamtindo  walipewa nafasi ya kubadilishana uzoefu  na watengeneza nywele hodari ambao Tanzania inaweza kujivuna nao.
Tukio hilo lilibarikiwa na uwepo wa mwakilishi wa Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Nnauye. Ambaye ni Mkurungenzi Idara Ya Sanaa na Utamaduni, Leah Kihimbi.
Mwakilishi mwandamizi wa kampuni hiyo hapa Tanzania, alizungumza kuhusu kundi hilo changa la Godrej Group lenye  miaka 119  likiwa na uongezeko la uwepo wake  barani Afrika, Amerika ya Kusini, na Asia.
Kundi hilo la Godrej Group ni wamiliki wa Darling Group katika nchi 14 za Afrika, ambapo Darling ni kiongozi wa soko la nywele na huduma za nywele.
Msemaji wa kampuni hiyo aliwakaribisha wageni waalikwa na kuwaambia  kuwa sehemu ya safari hii ya kusisimua nchini Tanzania, sababu bidhaa mbalimbali za Aliyana Professional ni kutokana na uimara wake.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top