Leo September 14 2016 Gavana wa benki wa Benki kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu
ameitoa taarifa kuhusu hali ya uchumi ambapo amesema uchumi wa nchi kwa
robo ya kwanza ya mwaka 2016 ukuaji wa Pato la Taifa unakadiriwa
kuongezeka kwa asilimia 5.5 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 5.7
kipindi kama hicho mwaka 2015.
Prof.
Ndulu ametaja vitu vilizochangia ukuaji huo wa uchumi kwa kiasi kikubwa
ni pamoja na kilimo (asilimia 11.7) biashara (asilimia 10.6), uchukuzi
(asilimia 10.1), sekta ya fedha (asilimia 10.1) na mawasiliano (asilimia
10.0). Shughuli za kiuchumi zilizokua kwa kasi ya juu zaidi katika robo
ya kwanza ya mwaka 2016 ni sekta ya fedha (asilimia 13.5), mawasiliano
(asilimia 13.4).
Akijibu baadhi ya malalamiko kuwa fedha kwa sasa imepotea Prof. Ndulu amesema ………>>>’hii
hisia ya kusema fedha imepotea, mimi nadhani kwenye hili ni muhimu
tukaelewa hisia zinakuja kwa sababu gani, serikali imechukua hatua kubwa
za kuongeza mapato kwa hiyo imeimarisha ukusanyaji kodi imeziba mianya
ya ukwepaji kodi’
‘Aidha
Serikali katika matumizi yake imebana shughuli za wale waliokuwa
mission town na shughuli hizi zilizo nyingi zinafanyika kwa uwazi‘
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )