Mwandishi : Eddazaria g.Msulwa
Ilipoishia....
.....Rahabu
akapunguza mwendo wa pikipiki na agnes akaruka na kukimbilia njia aliyo
kwenda kibopa,rahab akapita njia aliyo kwenda muntar.Muntar akajibanza
kwenye mti na kuokota gongo kubwa na kulishika kwa umakini.Gafla rahab
akajikuta akiichia pikipiki na kuanguka chini hii ni baada ya kupigwa
gongo la kifua na muntar akajitokeza mbele yake huku akiwa na gongo
mkononi....
Edndelea....
.....Rahab
akanyanyuka haraka,akamtazama muntar ambaye alianza kucheka kwa dharau
akimtazama rahab kuanzia juu hadi chini.Muntar akarusha gongo kwa
kutumia nguvu nyingi,rahab akalikwepa na kurusha teke lililotua shingoni
mwa muntar na akaayumba,kabla hajajiweka sawa rahab akampiga muntar
ngumi kadhaa za kifua na kuzidi kumfanya muntar kuyumba mithili ya mtu
aliyelewa kwa pombe za kienyeji.(mataputapu).
Muntar
akajaribu kurusha ngumi ila rahab akafanya maamuzi ya haraka katika
kuudaka mkono wake wa kulia,akajigeuza na kwakutumia bega lake akauvunja
mkono wa muntar.Kilio cha maumivu makali kikamkumba muntar.Pasipo kuwa
na huruma rahab akampiga mtama muntar na kumfanya aliachie gongo
alilolishika.Rahab akaliokota gongo na kuanza kumpiga muntar gongo la
kichwa hadi damu nyingi zikaanza kutoka nje kwa kasi kama bomba la maji
lililo pasuka sehemu ndogo.
Kibopa
akafunga breki za miguu yake baada ya kukutana uso kwa uso na
agnes.Kibopa akameza funda kubwa la mate huku mwili wake ukimtetemeka
kiasi kwamba akabaki akiwa hajajua nini la kufanya.Agnes akaachia
tabasamu pana baada ya kuiona surulia ya kibopa ikianza kuchora ramani
ya kutota kwa mikojo aliyo shindwa kuizuia.
“ni....Iisssa...Mehe”
Kibopa
alizungumza kwa kigugumizi kikali,agnes akapiga hatua hadi alipo simama
kibopa na akamtisha kama anampiga ngumi ya uso,kwa woga uliokithiri
ukammdondosha kibopa chini kama mzigo na akaanza kulia kama mtoto mdogo
“khaa wewe si jambazi,mbona unalia sasa?”
“mimi
ni nilikuwa kibaraka waoo tuu,sioooo jambaazzziiii” kibopa alizungumza
kwa kuyavuta vuta maneno kama amemeza fumba la uji wa moto na anashindwa
kuumeza.Agnes akamtazama kwa huruma kipopa ambaye taratibu alianza
kupiga magoti akimuomba msamaha.Agnes akampiga kofi la shavu kipopa na
kumuamuru kusimama
“wenzenu wapo wapi?”
“wameshakufaa”
“changanya mbaliga zako,kabla sijabadilika”
“eheee....!!”
Agnes
akampiga kibopa teke la makalio huku akimsindikiza na kofi la mgongoni
na kumfanya kibopa aanze kukimbia kwa kasi kubwa.Agnes akabaki kucheka
kwani hakutarajia kama ataweza kukutana na mwanaume muoga kama kibopa.
*****
Jackson
luther mpelelezi anaye sifika kwa kazi yake nzuri akaanza kupandisha
ngazi kwenda juu alipo anna kwa lengo la kumtia nguvuni kwa kosa la
mauaji.Anna akaanza kukimbia akipandisha ngazi kwa kasi hadi akafika
alipo waacha wezake.
“tuondokeni kimenuka”
Wakasaidiana
kumkokota fety ambaye amechoka sana kwa kazi ya kupambana na karim
pamoja na shamsa.Wakaingia ndani ya lifti na kushuka hadi gorofa ya
kwanza,jackson akaitoa bastola yeka na kuwa makini zaidi,taratibu
akaanza kuuunguza mwili wa muntar na kuhakikisha kwamba uhai wa mwili
huo umesharudi kwa Mungu baba.
Kitu
ambacho kinamchanganya jackson luther ni juu ya nani aliyeweza kumuua
karim kwani ni miongoni mwa majambazi ambao alijaribu kuwafuatilia kwa
kipindi kirefu pasipo kupata mafanikio ya aina yoyote katika kazi ya
uchunguzi wake.Akapandisha hadi gorofa ya tano alipomuona anna
akimalizikia na akakuta korido ikiwa haina mtu hata mmoja.
Akachunguza
sehemu yote na kumkuta mtu aliye anguka chini akiugulia maumivu na
mlango wa kuingilia chumbani kwake ukiwa upo wazi, akamsogelea na kumpa
mkono na kumuinua kutoka alipokuwa.
“umepatwa na nini?”
“kuna wadada bwana hapa,walikuwa wakipigana na kuniangusha”
“umeumia?”
“ndio nimepiga kiuno chini.”
“wameelekea wapi?”
“hata sijui wametoka vipi humu ndani kwangu”
“sawa”
Anna,fetty
na halima wakaingia kwenye jiko kuu la kupikia vyakula kwa kutumia
mlango wa chini wakashuka kwenye ngazi na kutokezea upande wenye
maswimcming pool katika hotel,wakawatizama watu waliomo ndani ya hotel
na kuona hakuna anayewatilia mashaka kwa mwendo wa umakini wakaanza
kuelekea kwenye sehemu lilipo gati la kuingilia hotelini.Kabla ya kutoka
nje ya geti walinzi wakawasimamisha,kwa jicho la kuiba fetty kwa
kupitia kioo cha dirisha la kijumba cha walinzi akaona video
inayomuonyesha akipambana na shamsa kupitia kwenye tv ndogo iliyopo
kwenye kijumba cha walinzi
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )