Lulu aliongeza kuwa wakati akifanya tukio hilo alikuwa ni msichana mwenye umri wa miaka 18, ambaye hakuwa na kazi na ilihita kiasi cha shilingi milioni moja na nusu kwa ajili ya kulipia ghalama za matibabu ya mama yake, pesa ambazo kama familia walikuwa hawana uwezo wa kuzipata.
“Unajua mimi nyumbani nimezaliwa mwenyewe, baba alifariki kitambo nikiwa mdogo na sina kaka wala dada, sasa mama yangu alipokuwa anaumwa wakati huo, kuna mzee mmoja mwenye uwezo tu nilikwenda kumuomba msaada ili anipe pesa nimpeleke mama hospitali, baada ya kumlilia shida alikataa kunisaidia bila kufanya naye mapenzi.
“Kwa kuwa nilikuwa ninashida ilibidi kukubali ili tu mama yangu apate matibabu lakini kiukweli, tukio hilo mpaka leo halijafutika akilini mwangu!” alimaliza Lulu Diva.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )