MWANDISHI : EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA...
“NDUGU
ABIRIA, NIFURAHA YANGU KUWA NANYI KATIKA SAFARI HII, NIMETOA LISAA MOJA
KWA KILA ABIRIA KUSALI SALA YAKE YA MWISHO KWANI NDEGE INAKWENDA
KULIPUKA NDANI YA LISAA HILO KUTIMIA KAMA HUAMINI, TIZAMA HII”
Samson
akaishika camera na kuigeuzia kwenye computer aliyo iietega mwendo kasi
wa saa, unao onyesha dakika zake zikirudi nyuma, kwani ikifika ndani ya
muda alio upanga, mfumo mzima wa ndege unakwenda kuzima, na litakalo
tokea hapo ni ndege kulipuka, jambo lililo anza kumuogopesha kila mmoja
aliyomo ndani ya ndege hadi raisi mwenyewe
ENDELEA...
Samson akaigeuzia kamera alipo na kuznedelea kuzungumza kwa sauti iliyo jaa msisitizo
“NAJUA
MUTASHANGAA, ILA NI KWAMBA NITAHITAJI RAISI KUFANYA HAYA YOTE AMBAYO
NITAMUAGIZA KUFANYA LA SIVYO PUUUUUUU, SOTE TUTAKUFA HAHAHAAAAA”
Samson
akaanza kucheka kicheko kilicho muacha mdomo wazi Rahab ambaye hadi
sasa hivi amuelewi Samson anamalengo gani na roho yake
Fetty,
Anna, Agnes na Halima hawatambui ni wapi wanapo elekea, kila mmoja
akabaki akiwa na wasiwasi moyoni mwake kwani, nyuso zao bado zimefunikwa
na vitu mifuko mnyeusi, isiyo wapa uwezi wa kuona kinacho endelea zaidi
ya pumzi zinazo ingia kwenye pua zao.Kila mmoja anahofu ya kuuliza ni
wapi wanakwenda kutokana kila jibu walilo pewa apo awali ni kwamba
wanaelekea kuzimu.Wakasikia mlango wa chuma ukifunguliwa kwenye chumba
walichopo.
“Yupi mkuu”
Sauti ya mwanaume ilisikika kwenye masikio yao, na hawakujua ni nani anaye uliziwa
“Huyu mwenye mahipsi makubwa”
Mkuu
wa askari alijibu kupitia redia ya upepo, huku akitazama kwenye moja ya
Tv iiyopo kwenye chumba chake, ikionyesha video za kamera za ulinzi
zilizopo kwenye chumba walichopo Fetty na wezake
“Ahaa sawa mkuu”
Askari aliye agizwa na mkuu wake wa kikosi, akamkamata Anna, na kumnyanyua juu
“Jamani munanipeleka wapi?”
Anna alizungumza huku akijitahidi kujitoa mikononi mwa askari huyo
“Tulia wewe, nitakuua malaya mkubwa wewe”
Askari huyo akamnyanyua Anna na kumuweka begani mwake, na kutoka kwenye chumba na kuuamiza mlango kwa nguvu
“Hakikisheni hatoki mtu hapa”
Askari
huyo aliwaagiza askari wengine wawili, walio simama kwenye malango
wakilinda chumba walichopo majambazi hawa wa kike.Askari aakendelea
kumbeba Anna ambaye anaendelea kufurukuta kwenye bega lake alipo muweka,
kutokana na ukubwa wa misuli yake iliyo jengeka vizuri kutokana na
mazoezi ya kijeshi anayo yafanya, Anna hakumsumbua kabisa kuchomoka
kwenye mikono yake.Wakafika kwenye moja ya chumba ambacho yupo mkuu wake
wa kikosi bwana Mathiasi Reymond na kumuingiza Anna na kumkalisha
kwenye kiti
“Tulia kama ulivyo la sivyo tutakunyonga”
Anna
aliendelea kupokea vitisho kutoka kwa askari aliye mtoa kwenye chumba
alicho kuwepo na wezake.Mathiasi Reymond, tayari amesha vua ngua zake na
kubaki na bukta yake ya ndani kwa ajili ya kufanya kazi moja tu,
yakumuingilia kimwili Anna, msichana mzuri aliye umbika kila idara ya
mwili wake.
Fetty
akanyanyuka kwenye kwenye sehemu aliyo kaa, lengo lake ni kusikiliza
kama atapokea amri yoyote ya kuambiwa kukaa kwenye sehemu yake, ila
ukimya ukatawala.Akapiga hatua za taratibu akizunguka kwenye chumba
akijaribu kujua ni kitu gani kinacho endela ila hakusikia chochote.
“Jamani mupo”
Fetty alizungumza kwa sauti ya chini
“Ndio, ila tupo wa tatu”
Halima alijibu kwa sauti ya kunong’oneza
“Nalijua hilo, Anna atakuwa amepelekwa wapi?”
“Yaani hata mimi mwenyewe sielewi?” Agnes alijibu
“Sijui hapa ni wapi jamani” Agens aliiuliza
“Cha msingi ni kujua nini tunatakiwa kukifanya na amini mumenielewa”
Fetty
alizungumza huku akijiegemeza kwenye ukuta wa chumba alichopo, kutokana
na mikono yake kufungwa kwa nyuma kwa pingu na kugundua si ukuta wa
kawaida
Mathiasi
Reymond akamuamuru mlizi wake, kumfungua vipingu za mikononi na
minyororo aliyo fungwa Anna kwenye miguu yake na mlinzi wake akafanya
kama alivyo agizwa na bosi wake.Baada ya mlinzi wake kumfungua Anna
akatoka ndani ya chamba na kumuacha bosi wake na Anna
Vichwa
vya viongozi wa pande zote mbili Tanzania na Marekani vinazidi kuuma,
kila mmoja akijaribu kutafuta mbinu na njia za kuweza kuipata ndege
yenye thamanini sana aina ya Air Force inayomilikiwa na serikali ya
nchini Tanzania huku ndani mwake ikiwa imembeba raisi pamoja na viongozi
wapambe wake.Juhudi za Satelait katika kuinasa ndege ya raisi na
kutambua ni wapi ilipo inafua dafu, jambo linalo zidi kuwachanganya sana
viongozi wa pende zote mbili.
Wanacho
kihofia viongozi wa nchini Tanzania ni kumpoteza raisi wao mpendwa
bwana Praygod Makuya, huku serikali ya Marekani ikihofia kupoteza moja
ya ndege zake ambazo ina uwezo mkubwa wa kuhimili mikiki mikiki ya vita
ya anga japo imetengenezwa kistarehe zaidi kwa ajili ya kumbeba raisi
huyu wa Tanzania aliye jijengea umaarufu mkubwa sana kutokana na ucheshi
wake na ushirikiano wake kwa wananchi na vingozi mbali mbali duniani,
katika mataifa tajiri na mataifa masikini
“Inatuazimu kutumia, mpango namba mbili(Plan B)”
Mkuu
wa jeshi la anga alizungumza na mkuu wa jeshi la anga nchini Tanzania
kwa kupitia mtandao wa kuonana moja kwa moja katika vioo vya Tv zao
kubwa zilizopo kwenye maofisi yao ya jeshi.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )