DA
ES SALAAM: Baada ya juzikati kupatikana taarifa kuwa mwanamuziki,
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amepatana na baba yake mzazi, Abdul
Juma, inadaiwa kuwa katika sherehe ya kutimiza siku 40 ya mtoto wa
Diamond aitwaye Nillan ‘Chibu Junior’, babu mtu huyo naye atatinga
Sauzi.
Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa Diamond
aliyeomba hifadhi ya jina lake, baba Diamond ni kati ya watu
watakaopata nafasi ya kukwea pipa kwenda Sauzi kwenye tukio hilo
linalotarajiwa kuchukua nafasi Januari 16, mwaka huu.
“Sherehe
ya kumtoa Nillan inatarajiwa kufanya Johannesburg, kule kwenye mjengo
wa Diamond. Watu kadhaa kutoka Bongo wakiwemo mastaa wamepewa mualiko na
utakuwepo usafiri maalum wa ndege wa kwenda na kurudi Sauzi.
“Nilimsikia Diamond akisema hata mzee Abdul atapata fursa ya kwenda kuwaona wajukuu zake, kwa hiyo tusubiri tuone,” alisema mtoa habari huyo.
Katika kuweka uzani wa habari hii,
mwandishi wetu alifanya jitihada za kumpata Diamond lakini simu yake
haikuweza kupatikana mara moja.
Ijumaa lilipata fursa
ya kuzungumza na baba Diamond na kuulizwa kama ana taarifa juu ya safari
hiyo ambapo alisema: “Hata mimi nasikiasikia ila kama itakuwa hivyo
litakuwa ni jambo zuri kwani nitapata nafasi ya kuwaona wajukuu zangu.
Kama nilivyosema, mimi na Diamond hakuna shida tena kwa hiyo hata hilo
la kwenda Sauzi linawezekana kabisa.”
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )