Msanii wa bongo fleva Madee amesema hajutii matusi yanayotukanwa
kupitia mitandao ya kijamii kuwa amepora simu kwa kuwa wanaomtukana
hawaujui ukweli na wakiujua watatulia.
Akionge kupitia eNewz Madee amesema
hajapora simu bali alikuwa anadai pesa ambayo aliitoa kwa
ajili ya kufanyiwa kazi na badala yake haikufanyika jambo lililomfanya
aende kwenye vyombo vya sheria kwa ajili ya kurudishiwa pesa yake, na
ndipo hayo yakatokea.
"Baada ya kuona pesa yangu ipo tu imekaa
hafanyi kazi yoyote, nikafuatailia sheria, nikaenda polisi, nikasaidiwa
kupata haki yangu, nashukuru nimepata haki yangu, wala sijutii
kinachoendelea, sasa mi naweza kupora simu rafiki yangu, mi natumia simu
yangi iPhone 7 na hiyo simu nayoambiwa nimepora ni S4, halafu kama ni
kupora nisingeenda na polisi" amefafanua Madee
Pia Madee amesema pesa yake huwa haipotei hata kama ikiwa imechukuliwa na maiti.
Hata hivyo Madee amesema uongo huwa
hauishi muda mrefu hivyo hawalaumu wale ambao wamemtukana kwa kuwa
hawaujui ukweli na anaamini kuna siku watu wote wataujua ukweli.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )