Mkongwe wa sanaa za maigizo nchini Mzee Jangala amewachana wasanii wa
kiume wanaovaa nguo zinazobana, kutoboa masikio na kuonesha maumbile
yao.
Akiongea
kupitia eNewz amesema vijana wanapaswa kujitambua na kuelewa maana ya
utandawazi na siyo kuiga mambo mbalimbali ikiwemo kukaa uchi mbele za
watu wazima kubadilisha maumbile yao halisi na kudai kuwa wanafuata
utandawazi na kupotosha jamii zima.
Hata hivyo Mzee Jangala hakusita
kuwasihi wasanii wa kizazi kipya kujitambua na kufanya mambo ya msingi
katika jamii kwa kuwa wao ni watu ambao wana mashabiki ambao
wanawaufatilia maisha yao na kuiga kila kinachofanywa na watu maarufu.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )