Serikali
imewasilisha pendekezo la mabadiliko ya Sheria ya Bodi ya Mikopo ya
Elimu ya Juu ili kuwezesha wanafunzi wanaochukua Stashahada katika
vipaumbele vya kitaifa, kupewa mikopo ya kuwawezesha kuchukua elimu
husika.
Waziri
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce
Ndalichako alisema mabadiliko hayo, yamelenga kuwezesha kasi katika
uchumi wa viwanda.
Profesa
Ndalichako alisema mabadiliko katika Sheria Namba 4 ya Mwaka 2016 ya
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), yamelenga kutoa
nafasi ya kada ya Stashahada inayohitajika ambao wamekuwa hawapati
mikopo.
“Kwa
lengo la kupata balance (mizania) na kwa kuwa Diploma nayo iko kwenye
elimu ya juu, watoto ni wale wale. Kuna wengine nao wanashindwa kumudu
gharama na ili serikali ipate uwiano mzuri tumeona ni vizuri kuwe na
marekebisho ya sheria,” alieleza Profesa Ndalichako.
Profesa
Ndalichako alisema kuna umuhimu mkubwa wa kada ya Stashahada, hasa
wanaokwenda sanjari na vipaumbele vya kitaifa kwenye msukumo wa Serikali
ya Awamu ya Tano wa ujenzi wa taifa la vijana, kama ilivyo kwa wenye
Shahada.
“Kama
taifa tunazungumzia uchumi wa viwanda,wadau wote hata wale wa ngazi ya
kati ni muhimu katika kuhakikisha kwamba ajenda hii inafanikiwa kama
vile ambavyo wale wa digrii wangelifanya,” aliongeza waziri huyo.
Mwaka
2004, kulikuwepo na mabadiliko katika sheria hiyo iliyowezesha
wanaochukua masomo ya sayansi, hisabati na elimu ya msingi (kwenye
msisitizo wa sayansi na hisabati), kupata mikopo ya elimu, nafasi
iliyoanza kutumika mwaka 2014, lakini hatua hiyo ilisimamishwa wakati wa
muhula wa masomo wa mwaka 2016/17.
Hata hivyo, HESLB ilikaririwa ikisema kwamba maamuzi ya kusitisha utoaji wa mikopo, ililenga kutekeleza maagizo ya serikali.
Hata
hivyo, jana Profesa Ndalichako alisema kwamba uamuzi wa kusimamisha
mikopo hiyo,ulitokana na nia ya serikali kufanya mabadiliko katika
sheria hiyo ili kuipa wigo mpana zaidi kuliko kujikita katika eneo la
sayansi pekee.
“Mwaka
2004 tuliingiza diploma, lakini kwa masomo ya sayansi pekee sasa,
tunataka kuwa na kipengele kinachopanua wigo ili tuweze kuhusisha kozi
nyingine za diploma ambazo zinaenda sanjari na vipaumbele vya kitaifa,” alifafanua waziri huyo.
Kwa
mwaka wa masomo 2016/17, serikali ilipanga bajeti ya Sh bilioni 483
ambazo zitakopeshwa kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wale
wanaoendelea. Katika mwaka huo, wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopata
mikopo walikuwa ni 25,715.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )