Watu
watano wamefariki dunia na 13 wajeruhiwa katika ajali ya gari
iliyotokea katika barabara ya Mwanza kwenda Shinyanga eneo la mtaa wa
Buhongwa Nyamagana mkoa wa Mwanza baada ya gari yenye namba za usajili
T.107 BKK Toyota coaster kugongana na Lori
Gari
hiyo aina ya Coaster ilikuwa ikiiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa
jina la Badru Habibu (33) mkazi wa Nyegezi na chanzo cha ajali hiyo
kimefahamika kuwa ni mwendokasi wa dereva wa Coaster aliyekuwa akijaribu
kuyapita magari ya mbele bila tahadhari na kusababisha vifo vya watu
watano na majeruhi 13.
Marehemu
waliofariki katika ajali hiyo hadi sasa ametambulika jina moja tu
ambaye ni 1. Abdul Mustafa, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya
42 hadi 45, huku marehemu wengine wa nne majina yao bado
hayajafahamika.
Aidha majeruhi wote kumi na tatu wapo hospitali ya rufaa ya Bugando wakipatiwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri, miili ya marehemu pia imehifadhiwa hospitali ya rufaa ya Bugando kwa ajili ya uchunguzi na utambuzi
Aidha majeruhi wote kumi na tatu wapo hospitali ya rufaa ya Bugando wakipatiwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri, miili ya marehemu pia imehifadhiwa hospitali ya rufaa ya Bugando kwa ajili ya uchunguzi na utambuzi
Kamanda
wa polisi mkoa wa Mwanza Naibu Kamishina wa polisi, Ahmed Msangi anatoa
wito kwa waendeshaji wa vyombo vya moto hususani madereva wa magari ya
abiria akiwataka kuwa makini pindi wawapo barabarani huku wakijua
wamebeba roho za watu, hivyo wazingatie sheria, kanuni na taratibu za
usalama barabarani ili kuepusha vifo na majeruhi ya aina kama hii
yanavyoweza kuepukika.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )