NABII Josephat Mwingira amedai
mahakamani kwamba hayuko tayari kupima kipimo cha DNA na hawezi kulipa
fidia ya Sh bilioni saba kwa sababu hajawahi kuzaa wala kuwa na
mahusiano ya kimapenzi na mke wa Dk. William Morris. Nabii Mwingira
alidai hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu
Mkazi, Godfrey Mhini alipokuwa akijitetea kuhusu madai dhidi yake
kwamba alizini na kuzaa na Dk. Philis Nyimbi ambaye ni mke wa Dk.
Morris. “Sifanyi vitu ambavyo sihusiki, aliyebeba mimba ndiye anajua
mtoto wa nani, amuulize mkewe mtoto kazaa na nani, uchungaji wangu ni wa
Mungu, siwezi kusafishwa kwa DNA,” alidai. Mahojiano ya Nabii Mwingira
na Wakili Peter Swai aliyekuwa akimuongoza kutoa utetezi wake yalikuwa
kama ifuatavyo: Swali: Tuambie cheo chako ni nani? Jibu: Cheo cha kiroho
ni Nabii na Mtume. Swali: Unafanya mahuburi wapi? Jibu: Efatha. Swali:
Unamfahamu Dk. Philis na Dk. Morris? Jibu: Nawahafamu wote, ni mtu na
muewe, walikuwa washiriki wa kituoni kwangu Efatha, Dk. Nyimbi ni mtoto
wa nyumbani, nilisoma na kaka zake, majirani kijijini kwetu. Swali:
Mnatokea kijiji gani? Jibu: Tunatokea Kijiji cha Mbaha wilayani Nyasa.
Swali: Kuna siku ambayo Dk. Morris alikuwa na ombi lolote kwako? Jibu:
Walikuja na mkewe kuomba msaada wa fedha kwa ajili ya kununua vitu
katika mnada bandarini? Swali: Shilingi ngapi? Jibu: Ni zaidi ya Sh
milioni 16, niliwapa kutoka katika akaunti ya Efatha, lakini mpaka leo
hawajarudisha. Swali: Hivyo vitu uliviona? Jibu: Niliviona, ni kama vile
vitu vinavyookotwa Marekani, nilishangaa anasafirisha takataka kutoka
Marekani mpaka huku. Swali: Ulishawahi kufuatwa na Morris kukulalamikia
kwamba una mahusiano ya kimapenzi na mkewe? Jibu: Ha ha ha ha, hapana.
Swali: Unafahamu kwamba Dk. Nyimbi ana mtoto? Jibu: Nafahamu. Swali:
Kuna siku hata moja aliwahi kukwambia baba wa huyo mtoto? Jibu: Hapana
hatujawahi kuongelea kitu kama hicho. Swali: Ulishawahi kuhusishwa
katika mgogoro wa mtoto wa Dk. Nyimbi? Jibu: Kwani Morris anasema mtoto
sio wake? Swali: Kuna tuhuma hapa, Morris anadai yule mtoto umezaa na
Dk. Nyimbi. Jibu: Niliwahi kusoma katika magazeti, sijawahi kuletewa
mtoto, lakini nikiletewa nitalea. Swali: Inasemekena wewe ulishiriki
katika kikao cha familia kilichotambua mtoto ni wako. Jibu: Hapana.
Swali: Kuna madai hapa mahakamani, Morris anaomba umlipe fidia ya Sh
bilioni saba kwa kuwa na mahusiano na mkewe, unasemaje? Jibu:
Tunaanzaje? Unapolipa lazima uwe umetumia kile kitu, hilo jambo halipo.
Swali: Unazungumziaje madai yaliyopo mahakamani? Jibu: Kama hii mahakama
inatenda haki, itaangalia kwa haki, Dk Morris atalipa gharama za
kunisumbua. Swai alimaliza kumwongoza mteja wake na mahakama ikatoa
nafasi kwa Wakili wa mlalamikaji, Respicius Ishengoma kumuhoji maswali.
Swali: Naomba nikuite Mchungaji? Jibu: Umetoa wapi hilo jina? Swali:
Nini tofauti ya Mchungaji na Nabii? Jibu: Mchungaji na Nabii ni tofauti
sana, kama ukisema hakimu na wakili, huoni tofauti? Kila mmoja ana kazi
yake. Swali: Ndiyo maana nimekuuliza kutaka kujua tofauti. Jibu: Mimi
nahubiri injili, sifanyi kazi moja tu ya kuchunga, ila nina wachungaji
chini yangu. Swali: Una watoto wangapi? Jibu: Nina watoto sita, lakini
mmoja marehemu. Swali: Wataja majina. Jibu: Lucy, Joshua, Anna, Jonath
na Glory. Swali: Glory alizaliwa lini? Jibu: Alizaliwa 2007. Swali:
Nikisema kazaliwa Mei 22 mwaka 2007 utakubaliana na mimi? Jibu: Mimi
niliyemzaa sikumbuki, wewe unatoa wapi? Alikuambia nani? Mimi siwezi
kusema nakubaliana na wewe. Swali: Unakumbuka mlifanya sherehe ya
kupongeza kuzaliwa kwa Glory Mei 22 mwaka huo na ukampeleka Dk. Nyimbi
Hoteli ya Millenium Tower?
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )