Jeshi la Israel limefyatua makombora kadhaa kuelekea eneo la Gaza, Palestina ikilenga wapiganaji wa kundi la Hamas.
Jeshi
hilo la Israel limeeleza kuwa katika mashambulizi hayo lilipiga maeneo
ya viwanda vya uzalishaji wa silaha na maghala ya silaha ya Hamas,
mapema leo. Hata hivyo, kwa mujibu wa Independent, makombora hayo
yalileta madhara katika maeneo ya makazi yakigusa pia watoto.
Hamaki
kati ya Israel na Palestina iliongezeka wiki iliyopita baada ya Rais wa
Marekani, Donald Trump kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.
Israel
imekuwa ikidai Jerusalem ni mji wake mkuu wakati Wapalestina
wakiendelea kudai upande wa Mashariki mwa mji huo kuwa eneo lao muhimu
lililotwaliwa na Israel katika vita ya mwaka 1967.
Jana,
kiongozi wa Hamas, Fathi Hammad alisema kuwa Taifa lolote
litakalohamishia ubalozi wake Jerusalem litakuwa ‘adui wa Wapalestina’.
Tanzania
kupitia Waziri wa Mambo ya Nje, Augustine Maige imeweka wazi msimamo
wake kuwa haitahamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem.
“Hatuna
ulazima wa kuhamisha ubalozi wetu. Unapaswa kufahamu kuwa ubalozi wa
Tanzania nchini Israel utabaki kuwa Tel Aviv na hakuna mpango wa
kuuhamishia Jerusalem ingawa kumekuwa na jitihada za kutushawishi
kufanya hivyo,” Waziri Maige anakaririwa na The Citizen.
Uamuzi
wa Trump umepokelewa kwa hisia tofauti na mataifa mengi huku ikielezwa
wazi kuwa utakwamisha mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )