Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ametuma salamu
za rambi rambi kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt.
Hussein Mwinyi pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance
Mabeyo, kufuatia vifo vya askari 14.
Spika
Ndugai amesema amepokea kwa masikitiko taarifa za vifo vya askari hao
ambao walikuwa wakilinda amani nchini Kongo, pamoja na wengine 44
waliojeruhiwa kufuatia mashambulizi yanayotekelezwa na askari waasi
nchini humo.
Kufuatia
tukio hilo, Spika Ndugai ametoa pole kwa familia za askari hao
waliouawa, na kuwaombea wale waliojeruhiwa kupona haraka na kuendelea na
shughuli za ujenzi wa Taifa.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )