Wajumbe
wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali shambulio
lililotekelezwa katika kambi ya walinzi wa amani iliyopo Semuliki, Kivu
Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kupelekea
vifo vya wanajeshi 20 huku wengine 53 wakijeruhiwa.
Kambi
ya jeshi hilo la ulinzi wa amani (MONUSCO) ilishambuliwa Disemba 7
jioni na kupelekea vifo vya wanajeshi 15 wa Tanzania na 5 wa DRC.
Wajumbe
hao wametuma salamu za pole kwa familia za wafiwa, serikali ya Tanzania
na DRC lakini pia MONUSCO huku wakiwatakia majeruhi afya njema na
wapone haraka.
Aidha,
katika taarifa hiyo wajumbe hao wameeleza kuwa kushambulia kambi za
walinzi wa amani ni tukio ambalo linachukuliwa kuwa ni uhalifu wa kivita
katika sheria za kimataifa na kwamba wahusika hawawezi kusamehewa kwa
matendo hayo.
Serikali
ya DRC imetakiwa kuhakikisha kuwa wahusika wa tukio hilo wanakamtwa na
kufikishwa katika vyombo vya sheria na kutaka makundi yote ya kihalifu
kusitisha mapigano.
Pia,
wamewashukuru wanajeshi na watu mbalimbali ambao wanahatarisha maisha
yao kila siku kwa ajili ya kuhakikisha amani inakuwepo duniani, na
kwamba tukio kama hilo la kusikitisha linaikumbusha dunia kuwa ni kiasi
gani watu hawa wameweka maisha yao hatarini kwa faida ya wengi.
Shambulio hilo la DRC ni kubwa zaidi kuwakumba walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa kwa miaka ya hivi karibuni.
Baraza
la Usalama alimesema kwamba litaendelea kushirikiana kwa karibu na
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa UN nchini DRC na MONUSCO kuhakikisha kuwa
wanatekeleza ipasavyo malengo yao.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )