Tume
ya Taifa ya Uchaguzi imeeleza kuwa inawashangaa viongozi wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanaosema kuwa hawamtambui mgombea wa
ubunge aliyesimamishwa kugombea katika jimbo la Singida Kaskazini.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Ramadhan Kailima ameeleza
kuwa CHADEMA kupitia Katibu wa Wilaya wa Singida Vijijini wamekamilisha
mchakato wa utambulisho wa mgombea wa Ubunge jimbo la Singida Kaskazini,
Joseph Njumbe
“Halmashauri
ya Wilaya ya singida wagombea 6 wameteuliwa juzi mmojawapo akiwa bwana
Joseph Njumbe wa CHADEAMA. Ameteuliwa kwa sababu amekidhi vigezo vya
kikatiba, kisheria na kikanuni yeye na chama chake cha Demokrasia na
Maendeleo.”
“Kwa
hiyo wanapolalamika kwamba huyu hawamjui nawashangaa sana. Nawashangaa
sana kwa saababu Kwa mujibu wa ibara ya 67 ibara ndogo ya 1b ya katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema Mgombea yeyote wa ubunge
lazima awe amependekezwa na chama cha siasa kilichosajiliwa.”
“Kanuni
namba 31 kanuni ndogo ya kwanza ya uchaguzi wa Rais na wabunge ya mwaka
2015, inasema mtu akitaka kugombea ubunge atawasilisha barua yake ya
utambulisho iliyosainiwa na katibu wa chama au wa wilaya wa chama
husika. Barua yake inawasilishwa kwa msimamizi wa uchaguzi.”
“Huyu
Bwana David Joseph Njunbe amewasilisha barua hiyo ya utambulisho
iliyosainiwa na katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Singida Vijijini, Bwana
Amani M mloya,” amesema Kailima.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi NEC, Kailima Ramadhani amesema kuwa kwa kupitia kanuni na
vigezo vya sheria ya uchaguzi, Mgombea huyo wa CHADEMA amekidhi vigezo
vyote vilivyohitajika ili kupitishwa kugombea Ubunge katika jimbo hilo.
Aidha,
Kailima ameeleza kuwa Joseph Njumbe, pamoja na kuwa ameshakamilisha
taratibu za kupitishwa kuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CHADEMA,
bado ana haki ya kikatiba ya kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho pale
tu atakapotimiza taratibu zinazotakiwa ili kujiondoa.
Kailima aliongeza kuwa Tume ya Uchaguzi haiangalii
“Sisi
hatuangalii muhtasari wa kamati kuu ama hatuangalii katiba
iliyosajiliwa na Katibu Mkuu wa chama chochote cha siasa. Tunaangalia
barua iliyosainiwa na Katibu wa Chama wa Mkoa ama Katibu wa Chama wa
Wilaya na ni kwa mujibu wa sheria, kanuni na maelekezo,” amesema
Kailima.
CHADEMA
pamoja na vyama vingine vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA)
vilitangaza kutokushiriki uchaguzi huo mdogo wa wabunge na madiwani
unaotarajiwa kufanyika Januari 18, 2018 ikidai kuwa mwenendo wa hali ya
kisiasa nchini siyo shwari na kuitaka Tume ya uchaguzi kuahirisha
uchaguzi huo.
Juzi
CHADEMA kupitia Mkuu wake wa Idara ya Mawasiliano, Tumaini Makene
ilitoa taarifa kuwa hakijateua mgombea wa ubunge katika Jimbo la Singida
Kaskazini na kumtaka Ndugu. Ramadhani Kailima kutambua kwamba mchakato
wa uteuzi wa mgombea wa ubunge ndani ya CHADEMA linasimamiwa na Kamati
kuu ya Chama hicho.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )