Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limepiga marufuku kufyatua
fataki siku ya mkesha wa sikukuu ya mwaka mpya hivyo wananchi
wametakiwa kukusanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo
Kawe ndipo wataruhusiwa kufyatua milipuko hiyo.
Kamanda
wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema upigaji wa fataki hizo umekuwa
ukifanyika kiholela na kusababisha baadhi ya wananchi kupata mshtuko
unaosababisha ugonjwa wa moyo
Mambosasa
amesema jeshi hilo limebaini siku ya mkesha wanapofyatua fataki hizo
baadhi yao wanatumia mwanya huo kufanya uhalifu na kupora mali
mbalimbali za wananchi.
Pia amesema baadhi ya watu wanatumia silaha za moto kusherehekea mwaka mpya jambo ambalo linaweza kusababisha vifo vya watu.
"Mwananchi
yeyote haruhusiwi kupiga fataki eneo lolote isipokuwa kwenye viwanja
hivyo wanapotakiwa kukusanyika na kupiga milipuko hiyo kwa nusu saa tu
ambapo ulinzi utaimarika siku ya mkesha wa mwaka mpya katika eneo hilo’’
amesema
Ametoa
onyo kwa mwananchi atakayeenda tofauti na hayo atakamatwa na
kuchukuliwa hatua za kisheria hivyo anayeruhusiwa kulipua milipuko ni
yule aliyepewa kibali maalumu na jeshi la polisi.
Pia
jeshi la polisi hilo limeweka mikakati ya kiusalama kwa ujio wa
maadhimisho ya sikukuu za Krismasi na mwaka mpya ili kuhakikisha amani
na usalama vinatawala wakati wa sherehe hizo.
Amesema
watashirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama ikiwa pamoja
na kikosi cha zimamoto na uokoaji,kampuni binafsi za ulinzi, vikundi vya
ulinzi shirikishi ili kuhakikisha wanathibiti matukio ya uhalifu.
Amesema
watatumia kikosi maalumu cha FFU, magari ya washawasha, mbwa na farasi
na askari wa usalama barabarani na makachero wamepewa maagizo maalumu ya
kuchukua hatua kabla ya matukio ya kihalifu kujitokeza.
Mambosasa
amesema zitatumika doria za miguu na pikipiki katika barabara zote
muhimu hivyo wananchi washerehekee sikukuu hizo kwa ngazi ya familia
katika mitaa kwa amani na utulivu.
Aidha
kikosi cha polisi wanamaji kitafanya doria kwenye fukwe za bahari na
maeneo ya jiji zima huku helikopta za polisi zikifanya doria kuhakikisha
usalama unakuwepo
"Polisi
watatoa ulinzi katika fukwe za baharini kwa kuweka vituo vya polisi vya
muda vinavyohamishika ili kutoa msaada wa haraka pindi unapohitajika,"
amesema
Pia
jeshi hilo limepiga marufuku disko toto katika kumbi mbalimbali
kutokana na sifa za kumbi zilizopo kutokidhi viwango vya kiusalama kwa
watoto
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )