Featured
Loading...

UVCCM nao waunda kamati kuchunguza mali za chama

Umoja wa Vijana UVCCM, umeunda kamati ya kufuatilia vitega uchumi na mali za umoja huo nchi nzima. Kamati hiyo inaundwa na wajumbe nane na itaongozwa na Mariam Chaurembo.

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka amesema kamati hiyo inakwenda kuchunguza na kuangalia vitega uchumi na mali zote za umoja huo.

"Mwenyekiti ameanza na kazi hii ili aweze kujua mali na vitega uchumi na umoja viko katika hali gani na vinaendeshwaje,"

"Wajumbe hawa watafanya kazi hiyo kuanzia leo wakiangalia na kufuatilia, kuchunguza, kuorodhesha mali za chama na mapato yanayotokana na vitega uchumi hivyo zinakwenda wapi," amesema Shaka

Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Peter Kasera, Zelote Saitoti, Rose Manumba, Sofi Kizigo na Elly Ngowi. Shaka amesema wajumbe wengine wawili watateuliwa kujiunga na kamati hiyo ambayo inaanza leo

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top