Jeshi
la Polisi limekwama kumhoji Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu
(Chadema), akiwa hospitalini Nairobi, Kenya baada ya kiongozi huyo
kusema kwamba polisi wa Tanzania hawawezi kumhoji akiwa nchini Kenya au
kwingineko nje ya mipaka ya nchi.
Kauli
ya Lissu imekuja siku 10 tangu Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon
Sirro, kuiambia Nipashe kuwa wametuma askari wawili kwenda Nairobi
kuchukua maelezo ya Lissu, baada ya Mbunge huyo kukubali kuhojiwa.
"Hadi
sasa Mwanasheria Mkuu wa Tanzania hajamwomba Mwanasheria Mkuu mwenzake
wa Kenya ruhusa ya mimi kuhojiwa na Polisi wa Kenya juu ya shambulio
hilo kama inavyotakiwa na sheria husika za nchi yetu," amefafanua Lissu
ambaye ni mwanasheria kwa taaluma.
Aidha
kwa upande wa IGP Sirro Alipoulizwa maoni yake juu ya kauli hiyo ya
Lissu kuwa polisi hawawezi kumuhoji nje ya mipaka ya nchi, aliiambia
Nipashe “Mimi sina jibu.”
Wiki
iliyopita, IGP Sirro alisema ametuma wapelelezi Nairobi baada ya
kusikia Lissu amekubali kuhojiwa juu ya tukio hilo na matarajio yao pia
ni kuwapata dereva na mlinzi wake.
“Tumetuma
watu wetu kwenda kuchukua maelezo yake (Lissu). Mwanzo tuliomba kwenda
lakini chama (Chadema) walikataa. Juzi tumesikia wamesema wapo tayari".
Sirro
Allifafanua
kwamba lengo kubwa ni kujua mazingira ya shambulio yalikuwaje na
kwamba ikiwezekana wampate dereva na msaidizi huyo wa Lissu ili
kurahisisha upepelezi wa tukio lenyewe.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )